Polisi wafukua mwili wa msichana aliyeuwawa na mpenziwe

kirinyaga1
kirinyaga1
Mwili wa mwanamke wa miaka 27 umefukuliwa kutoka kwa kaburi alilokuwa amezikwa ndani Kianderi katika kaunti ya Kirinyaga.

Eunice Wambui inadaiwa kuwa aliuwawa na mpenziwe wa miaka 35 Simon Murimi mapema wiki hili.

Maiti ya mwili huo sasa yamepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kerugoya huku polisi wakiendelea kutafuta mshukiwa mkuu.

Kina kilichosababisha mauwaji hayo hakijabainika wazi.