Polisi watawanya wafanyibiashara mjini Mombasa

teargas-415x260
teargas-415x260
Polisi mjini Mombasa wamewatawanya wafanyibiashara waliokua wakiandamana kulalamikia kubomolewa kwa vibanda vyao katika eneo la Buxton.

Hali ya mshikemshike ilitanda baada ya polisi kuwarushia vitoa machozi waandamanaji hao waliokua wameziba barabara na kuwasha moto, na kulemaza usafiri katika eneo la kuabiri magari ya kwenda mjini Malindi.

Wafabyikazi hao wanalalama kwamba maafisa wa kaunti walibomoa vibanda vyao bila sababu na wameapa kutobanduka kwani hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha.