Pombe ya Bure:Jamaa wakimbilia kupora  pombe baada ya lori la kubeba vileo kuanguka

Pombe
Pombe
 

Msiba wa mwenzio usiufurahie –lakini jumapili watu kadhaa walikiuka  kauli hiyop kwa kumbilia kupora chupa za pombe wakati  lori moja la kusafirisha  vileo kuanguka katika mzunguko wa westlands

Abiria ,wachuuzi na wahudumu wa matatu walikimbilia pombe hiyo  iliyotapakaa  baada ya ajali kutokea wakati dereva wa lori hilo alipopoteza mwelekeo  na kusababisha gari hilo kuanguka . Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa katika  tukio hilo .

" Hakuna watu wengi na nashangaa mbona polisi wametuzuia kuichukua pombe hii’ mtu mmoja aliyenufaika na pombe hiyo ya bure alisema . Polisi hata hivyo walifaulu kuokoa kreti kadhaa za pombe hiyo walipowasili katika eneo la mkasa .