eliud.kipchoge

Pombe yauzwa sh159 pekee ili kumshabikia Eliud Kipchoge

Kesho ndio siku inayongejewa na dunia nzima huku bingwa wa mbio za nyika, Eliud Kipchoge akitazamiwa kuivunja rekodi yake na kumaliza mbio za kilomita 42, chini ya masaa mawili.

Mbio hizo maalum zijulikanazo kama Ineos1:59 challenge zitafanyika Vienna, Austria kuanzia mida ya 7:45 asubuhi na Kipchoge atasindikizwa na zaidi ya waweka kasi 20.

Kipchoge akiri kuwa mtulivu kabla ya jaribio lake la Ineos1:59 challenge

Huku nchi nzima ikimuombea na kumtakia mema, vilabu kadha wa kadha vimeapa kuwapa mashabiki ofa baab kubwa ya bia ili waweze kumshabikia giwji wao.

Vilabu kama vile Blackyz, Cahoots na Moran Lounge wameapa kuuza bia zote kwa shilingi 159 ikiwa ndio masaa ambayo Kipchoge anatarajiwa kumaliza mbio hizo.

Kipchoge ambaye amekuwa akijitayarisha kwa zaidi ya miezi minne chini ya kocha wake Patrick Sang anasema ana imani ataweza kufaulu.

 Tazama picha zifuatazo.
159 2
159 159.3

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments