SUNSET:Mwisho wa safari ya Rais mstaafu Daniel Moi -1924 hadi 2020.

MOI
MOI
Daniel Toroitich arap Moi,  alizaliwa tarehe 2 septemba mwaka wa 1924  katika kijiji cha  Kabarak , taarafa ya    kaunti ya  Baringo  na alilelewa na mjombake Kimoi Chebii  kufuatia kifo cha babake aliyekuwa mzee . Alitoka  ukoo wa tugen  ambao ni sehemu ya jamii ya kalenjin .baada ya kumaliza masomo yake ya shule ya Upili  katika shule ya sekondari ya Kapsabet  alihudhuria masomo  ya ualimu katika chuo cha Tambach  katika wilaya ya Keiyo. Alifanya kazi kama mwalimu  kutoka mwaka wa 1946 hadi mwaka wa 1955 .

Mnamo mwaka wa 1955  Moi alijitosa katika siasa  alipochagliwa katika  bunge ili kuliwakilisha eneoe la Rift valley katika LEGCO.Aliteuliwa kuichukua nafasi ya  Dr.John Ole Tameno  mwakilishi wa zamani aliyeng’atuka maamlakani kwa sababu ya unywaji pombe kupindukia na kushukiwa kuhusika na vugu vugu la kupigania uhuru . Mwaka wa 1957  Moi alichaguliwa tena kujiunga na legco  na akawa waziri  wa elimu katika serikali  ya kabla ya Kenya kupata uhuru  kati ya mwaka wa  1960–1961. Mwaka wa 1960  alikuwa miongoni kwa walionzisha chama cha KADU  pamoja na Ronald Ngala  ili kupigania uongozi dhidi ya  chama cha KANU kikiongozwa na Mzee Jomo Kenyatta .KADU  ilipigania kuwepo kwa utawala wa majimbo ilhali  Kanu Ilitaka pawepo serikali ya muungano na utawala wa kikapitolisti . Kanu hata hivyo ilikuwa na uthabiti wa idadi ya waakilishi pamoja na kuungwa mkono na Uingereza amayo ilichukua hatua za kuondoa vipendee vyote vya majimbo katika katiba

Mnamo mwaka wa  1978 Moi alichukua usukani wa kuiongoza nchi wakati mzee Jomo Kenyatta alipoaga dunia .Aliongoza hadi mwaka wa 2002 alipostaafu . Kupitia shinikizo la mageuzi  ,Moi aliruhusu kuwepo mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka wa 1991  na kukiongoza chama cha KANU kupata ushindi katika chaguzi za  1992   na 1997 . kabla ya kuwa rais  Moi alihudumu kama makamu wa  rais  kutoka mwaka wa 1967 hadi 1978 .Moi alimua kuendeleza mfumo wa ‘nyayo’ ili kudumisha sera na mtindo wa utawala wa mtangulizi wake Mzee Jomo Kenyatta . Pia alipata jina la sifa kama ‘profesa wa siasa ‘  kwa sababu ya uongozi wake uliodumu miaka 24 na jinsi alivyokabiliana na wapinzani wake .Akiwa na umri wa miaka 95  Moi alikuwa rais mstaafu mwenye umri wa juu zaidi aliyekuwa hai. Februari tarehe 4 2020 ,Daniel Arapa Moi aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi . Mwezi uliopita madaktari katika hospitali ya Nairobi walilazimika kumrejesha Moi katika mashine za kumpa usaidizi wa kupumua .Hali yake ya afya imekuwa maaya tangu oktoba mwaka jana  alipolazwa hospitalini .

Wakati huo alipolazwa hospitalini ,msemaji wake Lee Njiru  alisema Moi alikuwa amekwenda hospitali kwa ukaguzi wa kawaida  lakini tangia hapo alilazwa hospitalini mara nne.  Kundi lake la madaktari likiongozwa na  Daktari  David Silverstein  limekuwa likimpa mkatibabu kwa matatizo yanayojirejeeza na kumfanya kusalia kitandani kwa miezi mitatu . Hali ya afya ya Mzee Moi ilizidishwa kuwa mbaya na  jeraha la goti alilopata wakati wa ajali iliyohusisha gari lake mwaka wa 2006 huko Limuru . Mzee Moi angetimu umri wa miaka 96 Septemba mwaka huu