'Punani' ya Madini Classic ipo YouTube, aogopa ichezwe redioni (+Video)

Screenshot_20190523_1739352__1570168627_21584
Screenshot_20190523_1739352__1570168627_21584
Staa wa muziki Madini Classic amedondosha nyimbo mpya 'Punani'

Katika mahojiano na Radio Jambo katika kitengo cha Papa Na Mastaa hususan Phone Call Ya Rais, staa huyu amesema kuwa haoni kuwa bodi ya kutathmini ubora wa filamu nchini inaweza kufungia nyimbo hiyo

'Punani' ni jina la msimbo linalotumiwa kuzungumzia sehemu nyeti za kike.

Alipoulizwa maana ya nyimbo hii, Madini alisimulia,

"Kila mtu anajua Punani inamaanisha nini. Hivi vitu ni kawaida tu. Mbona watu wanaogopa kusema vitu wanavyofanya gizani gizani?"

"Yaani kama mtu anataka kujua tu si anaweza google tu na ajue maana yake. Kila mtu mature anajua Punani inamaanisha nini..."

Madini amesema kuwa ngoma ilirekodiwa katika studio yake.

Soma hadithi nyingine;

"Ngoma yenyewe imefanyika kwa studio yangu tu. Unajua mimi nina ngoma nyingi. Nina ngoma kibao sana..."

Aidha, Madini hakusita kuzungumzia nyimbo iliyofungiwa ya Wamlambez. Staa huyu haoni sababu ya wimbo huu kufungiwa.

'Ni ile nilichagua mwenyewe nikaona mbona generation ya leo wanasikiliza Wamlambez sana mi nikaona nidondoshe hii."

"Wamlambez ndo aina ya ngoma zetu sasa ndo maana zinashabikiwa."

Madini alisema pia Willy Paul kutomhusisha katika kuipa nguvu Chuchuma sio kwamba hapendi ngoma hiyo,

"Ile ngoma binafsi naipenda sana . Lakini ukiona zile clips Willy Paul alikuwa anatafuta msanii na kumuambia vile anafaa kuifanya."

"Mimi kutoifanya sio kwamba siipendi au kwamba hakunimind.'

Madini pia alimzungumzia Noble Mirror92 msanii ambaye amemshirikisha katika ngoma hii.

"Huyo ni kama kakangu wa kitambo. Ni ile mtu nimeshinda nikimuona kutoka kitambo. Halafu kingine ni rapa mzuri kiukweli so kipaji kwanza."

https://www.instagram.com/p/B3H7BtmJ-FK/

"Ni msanii yuko pale studio kwangu kila siku..."

Aidha Madini amesema kuwa kwa sasa hana mipango ya kushoot video ya nyimbo hii.

Soma hadithi nyingine;

"Sijapangia Punani video bro..."

"Wacha tuseme hii ngoma ni ile ya kuimbia mpenzi wako .Hivi ni vitu watu wanaongea. Mimi sijaipeleka redioni."

Madini amesema kuwa haoni kuwa mtu yeyote anaweza akafungia nyimbo kama hii.

"Mi siwezi kujua. Atakayeifungia lazima atanipa sababu kwa sababu pia mimi ni msanii wa kenya."

"Ngoma mimi sijapeana ichezwe redioni nimeweka YouTube anayetaka kusikiliza akikosa sawa."