Raia Wanne wa Uchina wakamatwa kwa kumshambulia mhandisi wa Kenha

Wafanyikazi wanne raia wa Uchina wa kampuni moja ya ujenzi wamekamatwa huko Lodwar kwa kumshambulia mhandisi mmoja wa Kenya aliyekosoa kazi yao . Rodgers Imasia  ambaye ni mkaguzi  wa barabara kutoka KENHA Alivamiwa na wachina hao kwa kutilia doa kazi yao  ya ujenzi wa sehemu ya barabara ya  Loichangamatak – Lodwar.