Raila Junior aomba msamaha kuhusu matamshi yake ya ‘ODM slay queen'

Mwanawe kiongozi wa ODM Raila Odinga  ,Raila Junioe ameomba radhi kuhusu  ujumbe wake wa twitter ulioonekana  kuwakashifu viongozi wa ODM Kuhusu ajenda zao  . Raila Junior   jumanne alisema chama hicho kinafaa kurejelea mkono wake  wa hapo awali

"...  Chama chetu sio tu kuhusu ndege za kibinafssi na  Slay queens  na kuwatukana viongozi wengine ,tuna ajenda ya maendeleo  ambayo ipo katika manifesti yetu’ Raila Jr alisema

https://twitter.com/Railajunior/status/1306088096249896965

Lakini jumatano Junior alibadilisha msimamo wake akisema huenda ujumbe wake huo ulichukuliwa vibaya akisema ;

" Ufafanuzi …kama mwanachama wa kawaida wa ODM Maoni yangu  sio ya chama . Nakishukuru chama cha ODM  kwa kuruhusu demokrasia na kumpa kila mtu fursa ya kutoa maoni yake’ alisema

" Maoni yangu hayamlengi kiongoi yeyote  na naomba radhi  kwa  kutafsiriwa vibaya kwa ujumbe wangu’

Msamaha wake hata hivyo hakuchukuliwa kwa wepesi kwani watu wengi walionekana kuendelea kumkosoa wakimtaka akome kuzungumzia masuala ya chama cha ODM .

" Wewe na mjombako Oburu  mnafaa kujifiche sehemu Fulani hadi mikakati yote ianze kutekelezwa .. hamwezi kufunga midomo yenu’ @RealOmbatiEdwin said.

@patroba said " Ulisema ukweli . kwa kweli chama cha ODM  kinadidimia .huwezi kulinganisha ODM  ya mwaka wa 2007 na ODM YA 2020  mtu Kama Sifuna runs ODM like his pit latrine."