'Nilidanganya Mzee Moi kwamba nilikuwa bafuni' Rais Kenyatta awachekesha waombolezaji Kabarak

Rais Uhuru kenyatta leo ameongoza mazishi ya  rais wa Pili wa taifa Mzee Daniel Moi  huko kabaraka , Nakuru . Akimkumbuka Mzee Moi ,rais  amesema siku moja alikuwa  amefanya jambo ambalo mzee Moi hakulipenda . Pindi Mzee Moi alipojua kilichofanyika alimpigia rais Uhuru simu .

‘SIKU MOJA ALIPIGA SIMU…ASUBUHI..NIKAJUA HAPA MOTO UTAWAKA..NIKAMPA MAMA ACHUKUE ASEME NIKO MBALI .  BAADA YA DAKIKA TANO AKAPIGA TENA,NIKASEMA NILIKUWA NAOGA….MOTO UKAANZA….  BAADA YA DAKIKA KUMI AKAPIGA TENA NIKASEMA MZEEE SORRY …MZEE SORRY … AKASEMA NIENDE NIMUONE NAKURU CHINI YA SAA MOJA..NIKAJIAMBIA MJINGA TU  NDIO ANAJIPELEKA KWA MOTO…NIKALIWEKA SIMU CHINI NA NIKAENDA CHINI KWA WIKI MOJA HADI HIYO JOTO IPUNGUE …..’

Rais Uhuru aliongeza kwamba baada ya tukio hilo Mzee Moi alimsamehe na jinsi alivyokuwa mkali ndivyo alivyokuwa mkarimu  na mwepesi wa kusamehe . Kisa hicho kiliwapa kicheko sana waombolezaji wote waliohudhuria maazishi ya mzee  Moi .