Rais Kenyatta kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Magufuli

Picha kwa hisani ya: the-star.co.ke

Rais uhuru Kenyatta ametuma risala za kumpongeza rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa magufuli hivi leo. Taarifa kutoka serikali ya Tanzania imesema miongoni mwa marais wa Afrika wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ni Robert Mugabe wa Zimbabwe, paul kagame wa Rwanda na yoweri museveni wa Uganda.