Rais Magufuli awaleta pamoja Diamond, Alikiba na Harmonize

Wikendi iliyopita, Rais wa Tanzania Pombe Magufuli, aliwaleta pamoja wasanii wa bongo, Diamond Platnumz, Alikiba na Harmonize Kode Boy wakiwa katika hafla ya kuzindua chama cha kisiasa cha Chama cha Mapinduzi(CCM).

Wakati wa uzinduzi huo, Magufuli alihakikisha kuwa watatu hao wameketi pamoja na kutumia meza moja licha ya kuwa na lebo tofauti za mziki.

Kupitia hotuba yake Magufuli, alisema kuwa ana furaha kuwaona watatu hao wako pamoja licha ya kuwa na utofauti wao katika usanii wao, na anaamini kuwa chama cha CCM kina umoja mkubwa kuliko utofauti wa kila mmoja wao.

"Mimi nawashukuru sana wasanii. Unapomuana Alikiba amekaa pamoja na Diamond Platnumz unaiona nguvu ya chama cha Mapinduzi. Lakini unapomuana Harmonize aliyemkimbia Diamond Platnumz leo anamsifia hadharani huu ndio utanzania ninaoutaka." Alizungumza Magufuli.

Msanii Harmonize alipopewa fursa ya kuzungumza alimsifia Diamond huku akishukukuru lebo ya WCB kwa kumlea.

“Mimi naitwa Harmonize lakini mwanzo nilikuwa naitwa Rajab Abdul Kahali, mimi ni msannii ambaye nimeweza kuhangaika siku nyingi lakini namshukuru sana kaka yangu Diamond Platnumz, akanishika mkono na kunionyesha njia, akaniambia mdogo wangu pita humu. Kweli naushukuru sana na uongozi wa WCB ni kama walezi wangu. Na mimi nikaona kabisa nitakapopata nasafi na mimi nitashika vijana wenzangu mkono. So kwa heshima naomba nimtambulishe ambaye nimeshika mkono, siisi watu wa familia za kimaskini tuweze kusaidiana wenye kwa wenye. Kijana Mpya kutoka Konde Muisc Worldwide, Ibraah Karibu."

Wasanii waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na: Mbosso, Zuchu, Nandy,Lava Lava, Rayvanny, Shetta, Mwana FA,Babu tale miongoni mwa wengine.