Rais Mfu! Uchina yatuma madaktari Korea Kaskazini kuhusiana na hali ya afya ya Kim Jong Un

Kim-Jong-Un
Kim-Jong-Un
NA NICKSON TOSI

Taifa la Uchina limetuma madaktari katika taifa jirani la Korea Kaskazini kufuatia hali mbaya ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un ambaye amekuwa mgonjwa kwa muda.

Safari ya madaktari hao inajiri wakati ambapo ripoti kutoka kwa watu wa karibu wa kiongozi kuwa hali yake ya afya inaendelea kudhoofika baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Shirika la Reuters limeripoti.

Safari hiyo inasemekana kuwa imeongozwa na wakuu wa chama cha Kikomunisti cha Uchina kutoka Beijing Alhamisi kikielekea Korea Kaskazini kikiwa na maafisa wa afya wawili.

Alhamisi iyo hiyo kiongozi wa Amerika Donald Trump alinukuliwa akisema Kim hali yake ya kiafya ilikuwa imedorora na kukosa kuzungumzia iwapo walikuwa wamefanya mazungumzo .

Ijumaa, jamaa wa karibu wa Kim waliambia shirika la Reuters kuwa Kim alikuwa yupo hai na atafanya ziara mbalimbali kwa umma hivi karibuni.