Rais mstaafu Mkapa aliaga kutokana na mshtuko wa moyo-Familia yasema

Famillia ya rais mstaafu wa Tanzania marehemu Benjamin William Mkapa, walifichua haya wakati wa ibada ya wafu ilioandaliwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam Jumapili,26, Julai.

Rais wa muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli aliwaongoza watanzania katika hafla hiyo ya ibada ya wafu.

https://twitter.com/DannMwangi/status/1287312006366863360

Si mmoja wala wawili bali millioni ya wananchi wa Tanzania walifurika ili kuhudhuria hafla hiyo ili kumuomboleza rais mstaafu Mkapa na kutia familia yake nguvu

Mkapa atazikwa siku ya Jumatano nyumbani kwake Lupaso, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Kusini mwa nchi ya Tanzania.aliaga  dunia ijumaa iliyopita alipokuwa anapokea matibabu.

Hizi hapa baadhi ya ppicha za hafla hiyo;