'Rais tafadhali wafute mawaziri ambao wanafanya kampeni,'Waruguru asema

matiang'i
matiang'i
Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Laikipia Cate Waruguru amedai kuwa waziri Mutahi Kagwe na waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i wameenda kinyume na agizo la rais Uhuru Kenyatta la kuanzisha kampeni za siasa.

Akiongea Ijumaa Septemba 4 wakati wa hafla moja Laikipia, Waruguru alisema wawili hao wanataka Rais Uhuru kuwaunga mkono kugombea urais 2022.

Pia kiongozi huyo alisema ya kwamba uchumi wa nchi ni mbaya na wanapaswa kurekebisha na wala si kupiga siasa za mwaka wa 2022.

"Hali ya uchumi ni mbaya sana nchini na badala ya Waziri wa Usalama wa Ndani kuzunguka na kutathmini hali ili amshauri Uhuru kufungua shughuli za kiuchumi, ... yeye anatembea akikampeni kuhusu 2022

Rais tafadhali wafute kazi watu walio kwenye baraza lako la mawaziri na wanapiga kampeni za kugombea ugavana na urais 2022." Aliongea Waruguru.

Waruguru alisema kiboko kilichopewa Mwangi Kiunjuri kwa kukiuka  agizo la rais na kuenda mbele na kupiga kampeni za siasa kinapaswa kupewa mawazir hao wawili.

"Mtoto wetu Kiunjuri alidaiwa kupiga siasa na hivyo kufutwa kazi, sasa namuuliza Rais afanye hivyo kwa Matiang'i na Kagwe."

Kulingana na kiongozi huyo wa wanawake Mutahi amesahau kutekeleza jukumu la kazi yake wakati huu wa janga la virusi vya corona.