Rayvanny adondosha Remix ya Tetema na mastaa wakubwa Afrika

maxresdefault__1575371713_40132
maxresdefault__1575371713_40132
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rayvanny amedondosha remix video moto ya wimbo wake Tetema.

Kwa sasa Remix mbili zimefanyika za ngoma hii iliyotikisa Afrika nzima.

Katika kuhakikisha kuwa ameiteka soko la muziki Nigeria, Rayvanny amemshirikisha staa wa Nigeria Patoranking.

https://www.instagram.com/p/B5kQEYHA5ih/

Maneno yaliyotumika katika ngoma ya kwanza ya Tetema yalionekana machafu hivi kupelekea kufungiwa kwa wimbo huu hapa nchini.

Remix hii imewaleta pamoja Patoranking, Zlatan na Diamond Platnumz.

Ngoma hii inadondoka huku acapella ya Naogopa ikikubwa na ubishi baina yake na msanii chipukizi kutoka mkoa wa Iringa.

Aidha, Rayvanny ameshikilia kuwa Naogopa ni wimbo wake.

“Naogopa ni wimbo wangu. Ni utunzi wangu. Kila kitu nimeiandika mwenyewe. Nafikiria huyo dogo popote alipo anajua….” Aliendelea kuongea

Msanii huyu ambaye anafahamika kama Jimmy Msagala amesema aliamua kuufanya wimbo huu baada ya kumuona Rayvanny amelegea.

“Nilidhani kuwa Ray hana time nayo. Nikafika mkoa maeneo yangu ya kujidai na kuifanya nyimbo. Ni kweli ni kuwa nyimbo sio ya kwangu nyimbo ni ya Rayvanny…” Jimmy Msagala aliiambia Bongo 5.

Video hiyo ya dakika dakika 4 na sekunde 16 imefanywa na Cardoso Imeges.

Kupitia kibao hiki, Rayvanny ametimiza usemi wake wa kuifanyia Tetema remix na wasanii wakubwa Afrika.