Rayvanny atoa sababu za kumtaka Diamond Platnumz aoe Tanasha

Screenshot_from_2019_11_30_10_07_57__1575097768_74932
Screenshot_from_2019_11_30_10_07_57__1575097768_74932
Staa wa Bongo Fleva Rayvanny ametoa kauli kuwa Diamond Platnumz anatakiwa aoe Tanasha mrembo wa hapa nchini.

Rayvanny alitoa tamko hili katika 40 ya Naseeb Jnr katika Madale kwa Diamond Platnumz mjini Dar.

Sherehe hiyo ilijaa mastaa wa bongo na mashabiki wa msanii Diamond Platnumz.

 “Kila siku bosi tunakuja hapa kwa ajili ya sherehe za watoto tu, tumechoka sasa, ifike mahali uoe sasa,” alisema Rayvanny.

Rayvannny alisema kuwa muda unakwenda na sherehe za watoto wa Diamond zimekuwa nyingi ajabu.

Haya yanajiri huku ndoa ya Rayvanny mwenyewe ikionyesha dalili za kuvurugika.

https://www.instagram.com/p/B5dUpJqgEuh/

Wengi wanahoji kuwa kitendo cha Rayvanny kutoka kimapenzi na Nana kimefanya Fayma kumtema.

Aidha, mke wa staa wa muziki Rayvanny alisema kuwa Nana ana mimba ya miezi minne na ujauzito huo hauwezi kusingiziwa mumewe.

Akihojiwa na Global TV publishers, Fayma amlisema kuwa wanaomhusisha Rayvanny na mimba ya Nana hawana akili.

“Mimi siwezi nikazungumzia chochote na huyo mdada kwa sababu amefanya tu wimbo na baba mtoto wangu lakini vitu zingine sizijui…”

https://www.instagram.com/p/B5VABG3Jk5U/

“Ninachokijua ni kuwa ni mjamzito wa miezi minne niliambiwa hivo na mwanamume wake the day of the video alikuwepo akimsimamia akifanya video…”

Simba alipuuzilia mbali tamko la Rayvanny na kusema kuwa yeye ndiye anapaswa kumshauri kuhusu maswala ya ndoa.

Mondi alisema maneno hayo kutokana na skendo ya hivi karibuni kuwa Rayvanny alizinguana na mkewe Fahyma aliyezaa naye mtoto mmoja, kiasi cha kudaiwa kuwa wameachana.

Diamond Platnumz amezaa na wanawake tofauti tofauti akiwemo Hamisa Mobeto, Zari The BossLady na sasa Tanasha.