Rayvanny, Mbosso, Lavalava watakuja kuitema WCB. Afanyeje Mondi

diamond-platnumz
diamond-platnumz
Harmonize ndiye kifungua mimba cha lebo kubwa Afrika Mashariki ya WCB iliyopo mjini Dar nchi jirani ya Tanzania. Amekuwa mkubwa kwa kupiga nyimbo hatari na kushirikisha mastaa wakubwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Nigeria kati ya nyinginezo.

Matamasha anayoyafanya ni makubwa sawa na bosi wake Diamond Platnumz. Dogo ana mpenzi wa haiba ya juu sana Sarah. Ana walinzi sawa na idadi ya Diamond. Kumewahi kutokea vyombo vya habari nchini Tanzania zinazowalinganisha wawili hawa.

Soma hadithi hii:

 Diamond Platnumz alipuuzilia mbali kauli hii na kusema media zinajaribu ziwezavyo kukuza ubifu kati yake na wasanii aliowatengeneza. Juzi kati, Harmonize amedondosha barua na kuwapa kwaheri WCB.

Ila je, unaamini kuwa alichokifanya ni kitu kibaya. Mwana anapokua anatakiwa kujitenga mbali na babake mzazi na kuanzisha familia. Ndo maana staa huyu akaanzisha familia ya Konde Gang.

Soma hadithi hii:

Hii ni dalili tosha kuwa wasanii waliopo WCB siku moja watakuja kuwa wakubwa wote kama Diamond Platnumz na watataka kuwa huru kuanzisha lebo zao nje ya Wasafi. Kwa mfano, Lavalava ameanzisha Bite Gang, taarifa pia zipo Rayvanny anamiliki studio yake na ana wasanii dogo zake anaowapa mafunzo ya kuchana.

Soma hadithi hii:

 Diamond sasa anapaswa kuamua kati ya umeneja wa lebo na kuimba atachagua kipi? Kwa sababu wasanii waliopo WCB watatanua na kuanzisha lebo zao. Juhudi alizowekeza katika wasanii hawa ingawa zinamletea faida kuu, wasanii hawa watakua na hata kumshinda katika charts kubwa za muziki duniani.

Diamond ni mkubwa kweli. Anamiliki biashara kubwa kama runinga ya Wasafi, redio na nyinginezo. Ni msanii mkubwa Afrika na duniani. Ila achague afanye kitu kimoja. Hakuna mtu aliyewahi kufaulu katika mambo mengi. Una kauli gani kwake Diamond?