TANZIA, BRYANT: Ujumbe wa mwisho wa Bryant kabla ya kifo chake

Jumapili ,26,2020 ni siku ambayo mchezaji wa mpira wa kikapu Bryant Kobe alikumbana na mauti kupitia ajali ya helkopta.

Ajali hiyo ilitokea pale Kobe na Bintiye Gianna walikuwa safarini kuelekea katika Mamba Sports Academy eneo la Thousand Oaks, Carlifonia alikokuwa amepangiwa kufunza timu ya Vikapu ya shule alimokuwa akisoma bintiye Gianna.

Timu ya Gianna Mamba iliweza kucheza na timu mbili Jumamosi hiyo, katika ajali hiyo kulikuwemo  na Kocha wa timu ya Gianna mamba na  bintiye Byrant

"Kumpoteza Gianna ni jambo ambalo linaumiza moyo sisi kama wazazi, Mimi na mke wangu Michelle tunatuma rambirambi zetu na

pia tunaombea familia yote ya Bryant kwa msiba ambao umewapata na pia kumpoteza Byrant," Aliongeza Obama.

Rafiki yake Bryant Shaquille O’Neal hakuachwa nyuma aliandika ujumbe na kusema kuwa anampenda  Bryant na ni uchungu mwingi sana kumpoteza rafiki na ndugu wa karibu sana.

Alituma rambirambi zake kwa familia Kobe na pia kwa familia za waathiriwa wengine wa wa ajali hiyo.

Huu hapa ni ujumbe wa mwisho wa Kobe;