'Rudi Baringo ukapange huko kwanza,' Joshua Kutuny amwambia Gideon Moi

Mbunge wa Chereng'any Joshua Ktuny amemkashifu vikali mwekiti wa chama cha KANU Gideon Moi na kusema kuwa hawezi ongoza jamii ya Kalenjin na anapswa kurudi Baringo na kupanga watu wa eneo hilo kabla hajaanza kupanga jamii ya Kalenjin.

Kutuny alisema Moi anaongozwa na maslahi ya kibinafsi na hivyo hatilii maanani mahitaji ya jamii hiyo.

Pia Kutuny alisema kuwa Moi amekuwa akimchochea rais Uhuru Kenyatta kuwafuta wandani wa naibu wake William Ruto kazi walio serikalini.

"Tunataka kumuambia Gideon kuwa huwezi kuchukua nafasi kuadhibu na kutisha maafisa wa serikali ambao walipewa kazi  na Ruto au marafiki wake
Mimi nataka kumueleza Gideon kuwa kabla ya kuja hapa kutupanga na kupanga bonde la ufa, rudi kwako Baringo kwanza upange huko, ... kwa sababu huko ndio William Ruto ana umaarufu mkubwa. Ni kisa cha nyani ambaye haoni kundule." Alizungumza Kutuny.

Aidha amesema kuwa yuko tayari kuwasaidia na kuwatetea maafisa walioserikalini ambao ni wanadani wa William Ruto.

Inaarifiwa Kutuny walikosana na Moi kufuatia mabadiliko yaliyofanywa katika shirika linalosimamia ujenzi wa barabara za mashinani (KURA).

Mabadiliko hayo yalifanya Luka Kimeli, ambaye alikuwa ni meneja mkurugenzi, atimuliwe na nafasi yake kuchukuliwa na Philemon Kandie.