Ruto kama Donald Trump. Jinsi anavyotumia Twitter kukashifu habari 'feki'

untitled_design22_0
untitled_design22_0

Naibu wa Rais William Samoei Ruto sasa amegeuza mtindo wake wa kufoka au hata kuwajibu mahasimu wake wa kisiasa a na kugeukia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Hulka hii inafanana sana na ya Rais wa marekani Donald Trump.

Soma hadithi nyingine:

Kwa mfano, wiki hii Ruto amechapisha jumbe mbili katika mtandao huu.

Jumbe hizi zinaonyesha kero kubwa kwanza kwa gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru na vyombo vya habari.

Ya kwanza akimlenga Gavana Waiguru. Nyingine akilenga vyombo vya habari hususan gazeti moja la humu nchini.

Hii ni baada ya Gavana huyo mapema wiki hii kunukuliwa katika vyombo vya habari akisisitiza kwamba jamii ya Agikuyu haiko tayari kumchagua tena rais kutoka jamii hiyo.

Kauli hii ya Waiguru haikumfurahisha Ruto na akaamua kumjibu kupitia mtandao wa Twitter.

Soma hadithi nyingine:

“Tulimuunga mkono na kumpigia kura Uhuru akamrithi Kibaki kwa misingi ya uchapakazi wala sio ukabila. Yeye sio kiongozi wa jamii yoyote ila ni kiongozi wa Jubilee…” Ruto alisema.

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1172095736718209026

Tamko la Waiguru kwa kweli halikumgusa moja kwa moja Ruto wala hakutajwa popote. Ila kwa kusema hivyo anaweza kuwa akimaanisha kuwa katika miaka iliyopita jamii za Kalenjin na Kikuyu zilitawala Kenya na kwa hivyo Kenya haipo tayari tena kwa uongozi wa jamii hizi mbili.

Ruto anakimezea mate sana kiti hiki cha urais 2022.

Soma hadithi nyingine:

Siasa za ni nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta zinashadidi na kurindima kama moto jangwani licha ya Kenyatta kuwaonya wanaofanya siasa za mapema kukoma.

Hali hii imekigawanya chama tawala cha Jubilee katika tanzu za Kieleweke na TangaTanga.
Katika chapisho tofauti, Ruto anashangaa kuona jinsi waandishi wa habari wanavyoonyesha mgawanyiko katika  Jubilee. Ukimya wa rais Kenyatta kuhusu uteuzi wa Mariga unaonyesha uhalisia wa nyufa katika Jubilee.
"JUBILEE's Mariga is among 20 others. How can anybody contemplate our party,party leadership and machinery supporting any other candidate? The media should spare us these ugly shenanigans. The narrative is not funny let alone being newsworthy. Credit kenyans with some intelligence." Alichapisha Ruto.