Ruto ambaye amewahutubia wananchi katika mji wa Kisii amewarai watu wa eneo hilo kumuunga mkono huku akiwakumbusha kuhusu kampeini za Jubilee alizofanya wakati wa uchaguzi
Ruto amesema hatotikiswa na watu wanaomkosoa na kulemaza jitiahada zake za kufanya mikutano yake kwani kuna kazi nyingi ya kuwapa Zaidi ya vijana milioni sita kazi na kuwaondoa katika umaskini wakenya milioni 17 . Ruto amekashfu tabsha zilizotokea mjini Kisii kabla ya kuwasili kwake ambapo makundi ya vijana wanaopinga mkutano wake walipambana na polisi .
‘Kuna watu wanasumbua askari kuwaambia wasimamishe mkutano hii na ile ..hiyo ni ukumbafu’ amesema Ruto
Ameongeza kusema;
‘Wale wanasiasa wanataka kushindana na mimi Waachane na polisi wakuje kiwanja wakutanane na mimi’
Mji wa Kisii mapema alhamsi ulikuwa kitovu cha makabiliano kati ya makundi ya vijana waliokuwa wakiandamana dhidi ya Ruto na kundi jingine la kumuunga mkono . Ruto amedai kwamba vijana hao walikuwa wamelipwa kusababisha vurugu .
‘ Tumewaonyesha wale wanaotumia watu vibaya na kuwanunua vijana tunawaambia shame on you’ Ruto amesema
Ruto ameandamana na na viongozi mbali mbali akiwemo mbunge Sylvanus Osoro ,John Kiarie ,naibu gavana wa Kisii Joash Maangi, waakilishi kadhaa wa kaunti na viongozi mbali mbali wanaomuunga mkono .