SAD: Mwanafunzi Migori aaga dunia baada ya kunyongwa na andazi .

ndunya
ndunya

Mwanafunzi wa darasa la tano  katika shule ya msingi  Onyalo huko Migori ameaga dunia baada ya kusakamwa na andazi akijaribu kulimeza ili kulificha kutoka kwa wenzake .Josiah Ombura  alikuwa akicheza wakati wa mapumizko ya asubuhi wakati kisa hicho kilipotokea . ‘Marehemu alikuwa akiligawanya andazi moja ili kuwapa wenzake lakini wengi zaidi walipokuja aliamua kulimeza lote lakini likamsakama’ amesema mwalimu mkuu  Dedan Odhiambo.

Odhiambo  amesema wanafunzi wenzake waliripoti kwamba mwanafunzi huyo hakuweza kuongea  na alikuwa akijaribu kupumua .‘Ameripoti shuleni akiwa na furaha  na tukio hilo limetutamausha’ amesema mwalimu huyo mkuu .

.

Jaribio la kumfanyia huduma ya kwanza ili kumwokoa  na kumpelekea katika hospitali ya rufaa ya Migori limetibuka baada ya kutangazwa kuaga dunia alipofikishwa hospitalini . Chifu wa lokesheni ya Suna ya kati  Caleb Ombura  ambaye ni mjombake marehemu  amesema tukio hilo limewashangaza na polisi wataanzisha uchunguzi baada ya uchunguzi wa mwili kufanyika . Mwili wa mtoto huyo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya   Migori .