Safari za ndege ndani ya nchi zaanza rasmi

FILE PHOTO: Kenya Airways planes are seen parked at the Jomo Kenyatta International Airport near Nairobi, Kenya March 6, 2019. REUTERS/Thomas Mukoya/File Photo
FILE PHOTO: Kenya Airways planes are seen parked at the Jomo Kenyatta International Airport near Nairobi, Kenya March 6, 2019. REUTERS/Thomas Mukoya/File Photo
Kenya  imerejelea safari  za ndege ndani ya nchi huku ndege ya kwanza ya KQ ikianza safari  kutoka Nairobi kwenda Mombasa  Jumatano asubuhi.

Ndege hiyo ya  Kenya Airways  iliondoka uwanja wa JKIA   saa nne na robo  asubuhi  baada ya waziri wa uchukuzi James Macharia kuongoza hafla ya kuanzisha safari hiyo.

Ndege nyingine  ndogo ya KQ ilitoka Nairobi kwenda Kisumu

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari hizo, Macharia amesema  Kenya sasa inatarajia kuanza safari za kimataifa.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kwamba  safari za ndege ndani ya nchi zitaanza Julai tarehe 15 ilhali zile za kimataifa zitaanza Agosti Mosi. Safari hizo zitaendeshwa kwa kufuata masharti yote na mwongozo  wa wizara ya afya na mamlaka ya kusimamia safari za angani.

Uhuru  aliongeza kwamba  mahitaji zaidi ya kudumisha usalama wa kiafya wa wasafiri na wahudumu yatatekelezwa katika maeneo ya kuanzia safari na zinakotua  ndege. Mwezi Machi serikali ilifutilia mbali safari zote za ndege za ndani na  nje ya nchi