Safaricom yaondoa tozo kwa malipo ya mpesa ya kiasi cha chini ya 1000

Kampuni ya mawasiliano ya safaricom imeondoa tozo ya malipo ya mpesa ya  chini ya shilingi 1000 kwa sababu ya mkurupukonwa  virusi vya COVID19.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa amezirai kampuni za simu na benki kuzingatia kupunguza gharama ya malipo ili  kuwawezesha wakenya wengi kufanya malipo bila kutumia peasa taslimu kama njia moja ya kuzuia usambaaji wa virusi vya Corona .Zaidi ya watu 6000 wameaga duniakote ulimwenguni kwa ajili ya virusi hivyo huku Kenya ikithibitisha visa vitatu hadi kufikia sasa.

"Katika mkutano tumekubaliana kwamba kutuma  chini ya shilingi 1000 hakutatozwa  ada yoyote’ amesema afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Michael Joseph.;

Hatua hiyo inamaanisha kwamba kuanzia jumanne asubuhi watumiaji wa mapesa wataweza kutuma  kiasi chochote cha pesa chini  ya shilingi 1000 bila malipo katika sikun 90 zijazo .Joseph  amesema benkikuu pia imeidhinisha malipo ya kilasikuya mpesa hadi kiasi cha sasa cha shilingi elfu 70 kwa siku hadi shilingi elfu 150. Wakenya pia wataweza kufanya malipo ya mpesa ya hadishilingi elfu 300 kutika kiasi kilichozuiwa cha shilingi elfu 140 .