Sakaja kutoa ombi la kumzuia Mary Wambui kuchukua nafasi aliyopewa

Seneta wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja sasa anatoa wito kwa aliyekuwa Mbunge wa Othaya Mary Wambui kutochukua nafasi aliyopewa na rais Uhuru Kenyatta kuongoza mamlaka ya kitaifa ya uajiri.

Kupitia kwa taarifa kwa vyombo vya habari seneta Sakaja anahoji kuwa pana haja ya vijana kupewa nafasi ili kupunguza ukosefu wa nafasi za kazi miongoni mwa vijana.

Mamia ya vijana nchini wameendelea kulalamikia uteuzi wa Mary Wambui sawa na viongozi wengine katika nafasi serikalini huku vijana walio na tajriba wakiendelea kutaabika.