Sakata ya Kemsa! meneja mmoja alijaribu kusitisha ununuzi wa bidhaa kwa bei ghali lakini akapuuzwa

kemsa
kemsa

Mmoja wa mameneja wa Kepsa alijaribu kusitisha ununuzi wa bidhaa zisizofaa za Covid-19 kwa bei iliyoongezwa mwezi Aprili lakini akapuuzwa.

Mamlaka hiyo ilikuwa inaendelea tu kununua bidhaa hadi mwezi Julai wakati ilibainika wazi kwamba bidhaa hizo hazingehitajika, stakabdhi zilizowasilishwa kwa seneti na kufikia gazeti la

Kemsa ilinunua bidhaa za thamani ya shilingi bilioni 7.6 licha ya kuwa tu na ruhusa ya kununua bidhaa za thamani ya shilingi milioni 758.6 katika bajeti yake.

Kwa sasa shirika hilo lina bidhaa za thamani ya shilingi bilioni 6.2 katika hifadhi zake ambazo sasa linataka usaidizi wa wabunge kuzisambaza.

Mkurugenzi wa huduma za kibiashara Eliud Muriithi, aliyefika mbele ya seneti wiki iliyoplita alikuwa amehoji kuhusu ununuzi huo bila mpango na kwaa bei ya juu.

Katika barua pepe ya Aprili 24, Muriithi anaonekana kuonya wakurugenzi wengine wa Kemsa dhidi ya kununua bidhaa za Covid-19 kwa bei ya juu.

"Kutokana na upatikanaji wa bidhaa hizi, ikiwemo hata za kutengenezwa humu nchini kama vile maski tunafaa kutathmini upya bei za kuzinunua kwa ajili ya ununuzi bora," alisema.

Hata hivyo Julai 2, mkurugenzi wa ununuzi bidhaa Charles Juma, katika barua pepe kwa Muriithi na Jackline Mainye, alisema kwamba mchakato wa ununuzi wa moja kwa moja ulikuwa tayari umeanzishwa na kufanikishwa.

"Kutokana na hilo, tunakuomba utayarishe stakabadhi za ununuizi wa bidhaa zilizoorodheshwa na kuwasilisha shtakabadhi hizo kwa afisa mkuu mtendaji aidhinishe," Juma alisema katika barua ya Julai 14.

Muriithi hata hivyo alikataa. Alitaka kujua kutoka kwa mkuruugenzi wa ununuzi ni bajeti ipi iliyokuwa imetumika kwa ununizi wa bidhaa hizo.

Maswali hayo ya ununuzi na dosari katika ununuzi wa bidhaa hizo kwa sasa vinachanguzwa na tume ya maadili na kupambana na ufisadi.

Gazeti la The Star pia limebainisha kwamba tume ya EACC pia inawachunguza wanasiasa kutoka Jubilee na upinzani ambao huenda walihusika katika sakata ya Kemsa.