Sanda Ojiambo ateuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa jumuiya ya kimataifa inayoleta pamoja kampuni kufanya biashara

sanda-ojiambo-lise-kingo-e1590220258657
sanda-ojiambo-lise-kingo-e1590220258657
Sanda Ojiambo ameteuliwa kama mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya ya kimataifa inayoleta pamoja kampuni za kibinafsi na nyinginezo ulimwenguni kufanya biashara kulingana na vigezo vilivyowekwa na jumuiya hiyo almaarufu kama UN Global Compact.

Sanda kitinda mimba wa mwanasiasa Julia Ojiambo aliteuliwa na katibu mkuu wa jumuiya ya kimataifa Antonio Guteres na taarifa hiyo kutangazwa Ijumaa.

Sanda sasa ataanza rasmi majukumu yake mnamo Juni 17 wakati ambapo jumuiya itakuwa ikiadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa.

Taarifa iliyotolewa na UN imesema kuwa ni mwanamke wa pili kuchaguliwa katika kitengo hicho na atachukuwa nyadhifa zilizoachwa na Lise Kingo wa Denmark.

''She will bring 20 years of experience to lead the UN Global Compact in its next phase to mobilize a global movement of sustainable companies and stakeholders and bring the full weight of the private sector to achieve the Sustainable Development Goals (SDGs),” ilisoma taarifa hiyo.

Kabla ya kujiunga na Safaricom Sanda alikuwa anafanya kazi na mashirika ya kijamii chini ya vitengo tofauti.

Akifanya kazi na kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom,kampuni ya hiyo ilitia saini makubaliano ya kibiashara pamoja na UN ambayo yamechangia pakubwa ukuaji wa kampuni hiyo.

Anajiunga na shirika hilo ambalo kwa sasa lina washirika 10,000 wa kampuni ambazo zinatoka kwa mataifa zaidi ya 160