Sarah Wairimu akanusha taarifa za wasia wa Tob Cohen

roro_pix
roro_pix
Mjane wa Tob Cohen sasa anahoji kuwa taarifa za awali katika vyombo vya habari kuwa wosia wa kuiacha mali ya Tob kwa dadake sio kweli.

Sarah anasema Tob na yeye wanamiliki mali hiyo kwa viwango sawa.

Amekana taarifa kwamba dadake Tob anafaa kumiliki nyumba ya kifahari yenye thamani ya shilingi milioni 400.

Kupitia wakili Philip Murgor, Wairimu amesema kuwa alishangaa sana kuona habari hizo katika vyombo vya habari.

Mjane huyu anakabiliwa na tuhuma za kupanga njama ya kumuua mumewe.

Wairimu hakupewa ruhsa ya kukana au kukubali mashtaka.

Upande wa mashtaka umeomba muda kwanza ili afanyiwe vipimo vya afya yake ya akili.

Wakili wake Phillip Murgor aliiomba mahakama kumwachilia aende nyumbani kupigania haki zake za umiliki mali ya mumewe.

Murgor anasema kuwa mjane huyu ana haki tosha za kumiliki asilimia 50 ya mali iliyoachwa na mumewe.

Mahakama ilifahamishwa kuwa wahudumu katika jumba hilo tayari wametimuliwa na aliyekuwa mbunge Patrick Muiruri.

Upasuaji wa mwili wa Tob umepangiwa kufanyika hivi leo (Jumanne).