Sema Kurukwa! Gavana Tolgos asema hatamuunga mkono Ruto kuwa rais 2022

Gavana wa Elgeyo Marakwet  Alex Tolgos  ametangaza kwamba hatamuunga mkono naibu wa rais William Ruto kumrithi rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa wa 2022 . Kwa muda mrefu  Ruto amekuwa  na uhakika wa kuungwa mkono na viongozi wengi wa Rift valley na juhudi zake zimeelekezwa kutafuta  kura katika maeneo mengine ya taifa lakini sasa hatua hiyo ya Tolgos itapunguza kasi yake na kuvuruga   dhana yake kwamba ngome yake iko nyuma yake kwa njia thabiti . Tolgos amepuuza siasa za mapema za uchaguzi mkuu ujao akisema kama Jubilee ,suala kuu linafaa kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi .

‘Hatufai kufanya siasa kwa sasa kwa sababu kuna mengi ambayo serikali ya Jubilee iliahidi na  haijatekeleza.Huu sio wa wakati wa kukuuza maazimio ambayo hayajakomaa ya kupata uongozi’. Ameongeza kwamba uhusiano wake wa karibu na seneta wa Baringo Gideon Moi  haufai kuwapa watu wasi wasi kwa sababu  hauhusu siasa .