Sema kutoka mbio!Jamaa aliyedhaniwa kufa arejea nyumbani baada ya miaka 28!

shetani
shetani
Hebu  fikiria kumpoteza jamaa yako  kisha kuhudhuria maazishi yake  na  kila mwaka kufanya kumbukizi yake .

Halafu baada ya miaka 28 anajitokeza  ghafla nyumbani . Hayo ndio masaibu yaliyoikumba familia moja huko Shinyalu ,Kakamega  mwezi jana wakati  jamaa yao aliyeadhaiwa kufa  mwaka wa 1992 wakati wa uchaguzi mkuu aliporejea nyumbani  akiwa na mke na watoto wawili . Gilbert Shikwekwe  alikuwa akiishi Eldoret wakati huo baada ya kumaliza shule ya upili na jamaa zake hawakuweza kujua kilichomfanyikia walipokosa kusikia kutoka kwake .Baadaye zilizagaa ripoti kwamba alikuwa amegongwa na gari na mwili wake kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya  hospitali moja huko Kakamega . Jamaa zake walipanga maaazishi yake na kuuchukua miwili uliodhaniwa kuwa wake  kisha wakauzika na hata kusahau mambo yake .

Usitake kujua kuhusu mshutuko waliopatwa mwezi februari wakati wanakijiji waliomfahamu kwa sura na hata kuijua familia yake walivyoshangaa kumuona mtu kama yeye pamoja na mkewe na  watoto wao wakiingia kijijini humo . Wengi  walishangaa wasijue iwapo Yule alikuwa kizimwi  au  Gilbert na wengine waliacha shughuli zao ili kuwafuata nyuma pole kuona wataingia katika boma gani .

Vituko vilikuwa mbele na pindi walipoingia katika boma la mzee wake ,jamaa zake waliokuwa nyumbani wakati huo na waliomfahamu walianza kutimuka mbio kujiponya wakidhani yule alikuwa shetani amekuja kuwaandama!  Gilbert alijipata katika njia panda kuwaleza jamaa zake alipokuwa muda huo wote  lakini baada ya mabo kutulia na kila mtu kaketi kusikiza akawaambia kwamba muda  wa miaka 10 iliyopita alikuwa kafungwa jela huko Manyani ! amekuwa anje ya jela kwa miaka 18 na hata ameanza familia na ana watoto wawili  akiishi Mombasa .Wengi walishangaa jinsi alivyokuwa akiishi bila kutaka kuwaambia jamaa zake kwamba yuko hai au hata kuwaeleza wasiwe na hofu.Anasema alipotoka jela hakuna aliyefahamu kwamba  angepona na katika hali hiyo ndipo alipokutana na mke wake .Kabla ya kutaka kurejea nyumbani kwanza alitaka kuanzisha familia na kujipa uthabiti kidogo . Familia yake haikuamini kwamba ilimzika mtu aisyekuwa yeye katika boma lao na sasa wanatafuta idhini ya mahakama kuufukua mwili wa mtu aliyezikwa  akidhaniwa kuwa Gilbert .