Granton Samboja

Sema ukweli: Weka wazi uhalali wa vyeti vyako vya chuo kikuu

Kundi moja la wanaharakati katika kaunti ya Taita Taveta sasa linamtaka gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja kuweka wazi uhalali wa vyeti vyake vya chuo kikuu ili kusuluhisha mvutano ambao umekuwepo.

Msemaji wa kundi hilo la Taita Taveta Shadow Government Mohammed Washalla alisema kesi kuhusu vyeti alivyotumia Samboja kuwania ugavana inayoendelea kortini imeathiri pakubwa utendakazi wake na hivyo Kuna haja ya kujitokeza wazi kuelezea uhalali wa vyeti vyake.
Granton Samboja
Granton Samboja
“Kumekuwa na mdahalo mkubwa kuhusiana na makartasi yale gavana Granton alitoa ili apitishwe kugombania kiti cha ugavana kwamba si halali,
“Namwambia mheshimiwa gavana Samboja kumaliza mdahalo huu wote na kutunyamzisha, na kutoa shaka kwa wale walimpigia kura na wale hawakumpigia,
“Aje atueleze na kutuonyesha makartasi yake na tahasisi zichunguzwe,”Alisema Mohammed.
Samboja anadaiwa kughushi vyeti vyake vya chuo kikuu.
KATIKA KAUNTI YA KAKAMEGA: Nikuwa…
Huenda gavana wa kakamega Wycliffe Oparanya akaunda muungano wa kisiasa na naibu wa rais William Ruto kutafuta uongozi wa nchi hii katika uchaguzi ujao.
Wycliffe Oparanya
              Wycliffe Oparanya
Wabunge wa jubilee katika kaunti ya Kakamega Benard Shinali na Emmanuel Wangwe wameashiria ushirikiano huo.
“Aliniambia nikukaribishe kirasmi na akaniambia ako pamoja na wewe na muweze kukutana ili mpange jinsi kura ya kakamega itaenda kwako mwaka wa uchaguzi 2022,

“Viongozi wa Kakamega tumeweza kukutana na kujadiliana kuwa kura yetu tutapeleka mahali pamoja chini ya uongozi wa gavana Oparanya,”Walisema wabunge wa Kakamega.

RIP: Mauaji ya wakili Chesang kutokana na chachu za mipango ya biashara

“Natujue tunaenda wapi  na tunatika wapi kama nimeweza kuongea na rais,Raila na ninataka kukuhakikishia kura kakamega uko nazo tuko karibu kabisa,”Aliongea Oparanya.
Ni usemi ambao gavana Oparanya amesikika akiupigia upato.
lOVE: Mwanafunzi kuuwawa kwa kukataa uhusiano wa kimapenzi:
Kaiboi Technical Institute ilifungwa jana baada ya msichana wa mwaka wa kwanza katika shule hiyo kudungwa na kisu kifuani na shingoni na mwanaume ambaye alikuwa amemuuliza uhusiano wa kimapenzi na kukataa katika shule hiyo.

Msichana huyo, 21, alidungwa mara kadhaa alipokuwa amepiga foleni ili kuchukua kiamsha kinywa.

PHOTO: Legendary Dennis Oliech visits Joe Kadenge in hospital

OCPD wa Nandi Ezekiel Kiche alisema kuwa mwanaume huyo wa mwaka wa pili aliweza kuchapwa na wanafunzi wenzake baada ya kumuuwa mwanamke huyo na sasa yuko katika hali mahututi katika hospitali ya Eldoret.
Kiche alisema kuwa uchunguzi unaonyesha marehemu huyo alikuwa amekataa uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo.
“Aliweza kudungwa na kisu ya jikoni katika kifua na shingo mara kadhaa,” Aliongea mkubwa wa polisi.
Mwalimu mkuu Charles Koech alisema kuwa watafunga shule kwa siku chache ilikuwatuliza wanafunzi ambao walikuwa wanajaribu kufunga barabara ya Kaiboi-Mosoriot.
Waliweza kutolewa shuleni na polisi mara hiyo kisa hicho kilipotendeka.

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments