Serikali yakata bajeti ya shughuli zake, zikiwemo ziara za wabunge

Maafisa wa serikali wanafaa kujiandaa kwa wakati mgumu baada ya serikali kutangaza mikakati ya kupunguza matumizi ya pesa za umma.

Wizara ya fedha imetangaza kupunguza kwa kiasi kikubwa bajeiti za aidara za serikali hasa kwa safari za nje ya nchi na shughuli zingine za ofisi. Serikali ilitangaza kupunguza idadi ya magazeti katika idara zake, idadi ya ujumbe unaoondamana na mawaziri au makatibu wa kudumu wa wizara wanapokuwa kwa ziara za ugenini na matangazo katika vyombo vya habari kwa serikali kuu na zile za kaunti.

Hatua hii imechochewa na ripoti ya mdhibiti wa bajeti aliyetilia shaka ubadhirifu wa pesa katika idara za serikali kinyume na maagizo ya rais Uhuru Kenyatta. Waziri wa fediha Ukur Yatani amesema khatua hii itakuwa na athari kubwa na inafaa kuzingatiwa kila wakati.

Hali hii itaathiri idara ya mahakama, bunge, tume huru na idara zote za serikali ili kufanikisha kupatikana kwa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo kwa sasa imetengewa chini ya shilingi bilioni 700 kwa bajeti ya shilingi trilioni tatu.

Yatani amesema ni maafisa wanne pekee watakao kuwa katika ziara za ng’ambo za mawaziri ikimjumuisha waziri mwenyewe.

Ujumbe wa katibu wa kudumu utakuwa na watu watatu pekee na ziara hizotitu ikiwa afisa anayehusika atathibitisha umuhimu au manufaa ya ziara hiyo kwa taifa la Kenya.

Ziara zote za kuzuru maeneo mbalimbali kujifunza vile mambo yanavyotendeka zimefutilwa mbali mara moja hadi pale serikali itakapotangaza kuzirejesiha tena. Marufuku hii pia inajumuisuha safari za wabunge.

Yatani ameshauri wizara na idara za serikali kutumia teknolojia ya kisasa katika sekta ya mawasiliano kuendesha shughuli zao na kuwasiliana na wawekezaji wa kimataifa. Pia anawautapka kutumia balohzi za Kenya katika nchi husika bahdala ya kulazimika kusafari.

Data ya mdhibiti wa bajeti iliyoonyesiha kuwa jumla ya bajgeti za usafiri katika serikali ilienda juu kwa asilimia 67 hadi shilingi bilioni 15kufikia mwezi Juni mwaka jana.

Mafunzo yote kwa maafisa wa serikali yatafanyiwa humu nchini isipokuwa maafunzo maalum.

Madereva wa magari ya serikali pia watahitajika kuyaendesha katika muda unaoruhiwa kisheria.