Serikali yataka watu wanunue sanitizing towels ,nani atasaidia Chokoraa Jamani?

90056264_2291587394476687_3957723962897288600_n
90056264_2291587394476687_3957723962897288600_n
NA NICKSON TOSI

Mwanawe gavana wa kaunti ya Nairobi Saumu Sonko amekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki za watoto wanaoranda randa mitaani almaarufu kama chokoraa ,na sasa anasikitika kuwa huenda watoto hao wataathiriwa pakubwa kutokana na virusi vya Corona ambavyo vimevamia taifa la Kenya na mataifa mengine takriban 123 ulimwenguni.

Kulingana na Saumu watoto hao hawana makaazi maalum ambayo yanaweza kuwakinga dhidi ya virusi hivyo na hata hawana uwezo wa kupata maji ya kuwawezesha kunawa mikono jinsi wanavyopendekeza maafisa wa afya nchini.

Saumu aidha anashangazwa namna serikali imedinda kutoa vitambaa ama sanitizing towels kwa watoto hao ambao hawana uwezo wa kununua vitambaa hivyo.

Wakati ulimwengu ulikuwa ukiadhimisha siku ya wapendao ,Saumu alichukuwa fursa yake na kutangamana na watoto hao katika mitaa mbali mbali ambapo aliwanunulia vyakula ,nguo na kuwapa hela kidogo za kuwakimu.

Swala la Virusi vya Corona kutua nchini ,limeonekana kuatua moyo wa Saumu ambaye ameirai serikali kuwasaidia wakenya hao ambao hawana uwezo wa kununua vitambaa hivyo vilivyopendekezwa na wizara ya afya.

"sasa ni nini ambacho kitafanyika kwa watoto wa kurandaranda mitaani wakati ambapo serikali imepgia marufuku watu kuwa katika vikundi?,ni wapi ambapo wataenda iwapo watahisi kuwa wagonjwa na ni nani ambaye watamfikia ndiposa wapate matibabu,na ni vipi watapata vitambaa vya kujkifunika uso?.aliandika Saumu.

Saumu kabla ya kujabarikiwa mwanawe wa pili alikuwa anaamka majira ya asubuhi na kuanza kuwapigia watoto hao wa kuranda randa mitaani chakula,kitu ambacho kulingana na yeye ni kizuri ikilinganishwa kuwa ni watoto ambao wanahitaji usaidizi kwa jamii.