'Shemeji alimtoa bwanangu kwa ndoa kupitia uganga,' Asema mwanadada

Massawe
Massawe
Katika mjadala ambao wanajambo walisimulia jinsi wamejihusisha na mambo ya uganga au jinsi imewaathiri.

Mwanadada mmoja kwa jina Josephine alisimulia jinsi shemeji yake alivyomtoa mumewe kwa ndoa yao na kumfanya aoe mwanadada mwingine.

Kulingana na Josephine, shemejiwe alienda kwa mgongo na kupewa madawa ambayo alimpea mwanadada fulani na kumueleza amwekee bwanake. Baada ya hayo, yule jamaa maskini wa mungu alimfuata mwanadada na wawili hao wakafunga ndoa.

Isitoshe, Josephine na bwanake walikuwa wamejaliwa watoto wawili.

Sasa imetimia miaka mitano na wawili hao tayari wamejaliwa mtoto mmoja.

Uzuri ni kuwa mumewe sasa ameanza kurudisha fahamu na amepanga kumtembelea mkewe Jumamosi hii na mkewe Josephine anakiri kuwa bado hajawacha kumpenda.

Soma usimulizi wake.

Mimi sijawahi enda kwa mganga lakini shemeji yangu alienda kutoa mume wangu side yangu.

Wakati alimtoa alienda akatafuta msichana akampa madawa ili amuekee bwanangu ili waishi pamoja, na mpaka sahii wameishi kwa miaka mitani na wana mtoto mmoja.

Nina mika mitano tangia nitolewa kwa ndoa yangu na naweza rudiana na mzee wangu kwani yeye hajui kama ni makosa na hajiui nini inaendelea.

Nilimwambia kilicho tendeka na hata ilifika mahali akaanza kujua na akaanza kujitenga na dadake. Last Disemba alimpigia dadake akamwambia wewe ndiye ulitenga ndoa yangu na nataka urudishe mke wangu.

Hata sahii nazungumza na wewe naona nikama zile nguvu zinaisha na hata alini promise anakuja Saturday.

Tulizaa watoto wawili na bwanangu.