Siku imewadia! Mbusii kutuzwa katika hafla ya nne ya Africa 35.35

Siku tulioingoja kwa hamu na ghamu kama familia ya Radio Jambo basi imewasili!

Siku ninayoizungumzia ni ambayo mtangazaji Daniel Githinji Mwangi, almaarufu Mbusii deh wa kipindi cha Mbusii na Lion teketeke, atakuwa akituzwa.

Mbusii atakuwa akituzwa katika hafla ya nee ya Africa 35.35 awards ambayo itafanyika hii leo na kesho katika nchi ya Ghana, magharibi mwa Africa.

Tuzo hizo huwatambua vijana Afrika nzima kuanzia miaka 18 hadi 35 na Mbusii ndiye atakayepokea tuzo la muafrika bora katika nyanja ya utangazaji aidha redioni au TV.

Soma barua kutoka wasimamizi wa tuzo hilo.

Dear Mr. Daniel Githinji Mwangi, The “Africa 35.35 Awards” is an initiative that rewards outstanding young personalities from Africa and the Afro-Diaspora aged 18 to 35, transforming our continent with their exceptional contributions. We are delighted to announce your selection as Laureate of the 2019 edition in the category «Best African Act / On Air Personality (TV/Radio)».

The 4th Edition of the Laureates Leadership Program and the Awards ceremony will be held at the renowned Swiss Spirit Hotel & Suites Alisa in Accra – Ghana, on November 24th and 25th, 2019. Supported by various African partners and media, our Awards represent today a prestigious annual event that celebrates the merit and excellence of youth of African descent. 

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Mbusii aliwajulisha mashabiki wake kuwa tayari ameondoka nchini kuelekea Ghana, huku akimshukuru maulana kwa tuzo hilo.

Mbusii aliandika,

Safari ya Ghana imeanza, 35.35 African award. Best radio personality in Africa 2019. Thanks to most high Jah.

Tunamtakia a mbusii deh kila la heri na tunampongeza kwa kazi safi!