Siku za mwizi ni Arobaini! Picha za tapeli Peter Wanjau aliyekuwa anajifanya mfanyakazi wa runinga ya Citizen kuwatapeli watu

Wahenga hawakukosea waliposema kuwa siku za mwizi ni arobaini tumesikia Wilkins Fadhili ambaye alifichuliwa na wasanii kwa kuwatapeli watu, pia tumemsikia Waswa ambaye alikuwa anazungumza kama rais Uhuru Kenyatta sasa ni Wanjau.

Peter Wanjau ambaye anaishi katika kaunti ya Nakuru amekuwa akiwatapeli wananchi kwa kusema kuwa ni ripota wa runinga ya Citizen. Amekuwa akichukua pesa kutoka kwao na kuahidi kuwa habari zao zitakuwa katika runinga hiyo.

Jumanne, Wanjau na wenzake wawili ambao wamekuwa wakijifanya wafanyakazi wa runinga hiyo, Doreen Waiganjo na Githaiga Karanja, walikamatwa walipokuwa wanataka kufanyia mahojiano au kumtapeli aliyekuwa bosi wa NACADA John Mututho.

Akizungumza na runinga hiyo alikuwa na haya ya kusema;

"THEY STARTED CONTACTING ME TODAY MORNING AT AROUND 8 A.M. AND BY 10 A.M., THEY HAD MADE AROUND 10 CALLS. THEY WERE PUTTING PRESSURE ON ME AND TOLD ME THAT THE REPORT WAS NEEDED FOR THE 1 P.M. BULLETIN…I WONDERED WHY THEY NEEDED CORONAVIRUS-RELATED INFORMATION FROM ME."

Mututho alijua kuwa mambo si mema hapo ndipo alipopiga simu kwenye runinga hiyo.

Wanjau alishtakiwa kwa kuwatapeli watu kadhaa katika mji wa Nyeri, Nairobi na Nakuru huku mmoja wa waliotapeliwa akiwa mama wa mtoto anayeugua saratani.

Katika mitandao yake ya kijamii, picha zake nyingi amepigwa akiwa na wanasiasa, wasanii, wacheshi na hata watu mashuhuri. Wananchi walioghadhabishwa na tendo hilo walikuwa na haya ya kusema;

Umwami Tz Hiyo story ya kale katoto kagonjwa, I can conclude that humanity has lost it’s way.

Paul Waiganjo I know this guy. He tried to con me but God saved me from his hands.

Dalmas Mutai So unfortunate on the sick girl.

Stanley Malumbe Very shameless.. someone dying of cancer and you busy taking advantage.. this person should be hunged if not jailed for life.

 Tazama picha zake Peter Wanjau;