Simon Mbugua aipeleka CBK mahakamani

unnamed (3)
unnamed (3)
Mbunge wa EALA, Simon Mbugua amefika kortini kupinga uamuzi wa Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Partrick Njoroge kuidhinisha noti mpya zitakazotumika hapa nchini.

Njoroge alihoji kuwa juhudi hizi zinafanyika ili kupunguza viwango vya ubadhirifu wa hela nchini na ufisadi ambao umelemaza juhudi za serikali katika kuaafikia malengo yake.

Hali kadhalika gavana huyu anasema kuwa anafuata sheria katika katiba mpya iliyoidhinishwa 2010 na Rais mstaafu Mwai Kibaki kuzibadilisha mwonekana wa hela inayotumika nchini.

Pata uhondo hapa:

Noti za awali za elfu moja zitagoma kutumika tarehe mosi Oktoba ili kupisha noti mpya ambazo zilionyeshwa katika sherehe za Juni mosi za Madaraka. Mbunge huyu anateta kuwa Benki Kuu ya Kenya haikuwahusisha wakenya katika mchakato mzima kuanzia kwenye uchapishaji hadi kuja katika kuzionyesha hadharani.

Soma mengine hapa:

Anaitaka mahakama kusimasisha juhudi za kuzifanya noti hizo kuwa halali kutumika hapa nchini mara moja kesi ikusubiria kusikilizwa. Anateta pia kuhusu picha ya Mzee Jomo Kenyatta akisema kuwa uwepo wa picha hiyo katika noti hizo inaenda kinyume na katiba iliyopitishwa 2010.

Mtetezi wa haki za wananchi, Okiya Omtatah pia yupo na maoni yale yale yake Simon Mbugua na muda mfupi ujao anasubiria kuiburuza CBK mahamakani ili kusimamisha mchakato mzima wa kuidhinisha noti hizo.

Mengi yanafuata...

Hadithi imehaririwa na kuchapishwa na Abraham Kivuva.