Sio Kwamba Nataka Kujionyesha Ninapoweka Mambo Yangu Mitandaoni, Nyota Ndogo Asema

18556210_1203276633114185_824090735604703862_n
18556210_1203276633114185_824090735604703862_n
Mtandao wa Facebook ni jukwaa ambalo bila shaka kila mmoja hulitumia kujieleza. Hasa kwa wasanii jukwaa hili huwasaidia kuwafikia mashabiki zao, kuwauliza maoni kuwahusu na mambo mengi tu

Kwa msanii Nyota Ndogo, mwimbaji wa wimbo 'Kuna watu na viatu' , mambo sio tofuati. Yeye huuliza maoni kutoka kwa mashabiki zake kuhusu mambo mengi sana ikiwemo maswala ambayo kwa wengine wanayaona kuwa ya kibinafsi sana.

Hivi karibuni ameuliza mashabiki zake maoni yao kuhusu shamba alilotakakununua.

 Jamani kuna hii shamba nimekwenda kununuliwa leo wapenzi.nimefika nimeona nimependa heka mbili.ila nimegeuza roho nilipofika maana mimi sio mkulima kisha mda wangu mwingi wausafiri kazi na mziki.sasa sinitaibiwa mimi vyakula baada nipate faida nipate haraka mpaka mtu akuulize nilinunua hasara.vizuri nijijue tu kua sitakua na mda na shamba.itanipa stress kwakweli.NYIE LEO MUNI ADVICE PLZZ.nimerudi kufikiria tena home.

Kama unafikia kwamba watamkashifu kwa kuweka maswala kama haya mtandaoni umenoa.

Haya hapo ni baadhi ya maoni ya mashbiki wake;

 Nyota nunua dada unaeza eka mtu a manage then later kama haileti faida,unaeza uza ununue plot place poa ueke rentals na jina yawatoto itawasaidia wakiwa university.

Keti chini nikupe advice

Sasa hapo shambani kapande mbuyu... Mkorosho

Hutakuwa na wasiwasi hata ukisafiri mwaka nzima. Pili... Mziki kaimbe kwa instagram na sisi tutakufollow kwa tweeter.. Shughulika na ukulima. Mwanamke ni jembe dada...

Shamba ni kitu inapanda value daily..nunuliwa achana nayo ikae baadaye unaeza iuza mamilioni

Nunua the value will go up u will sell later

Nilitaka kujua kutoka kwake iwapo yeye huzingatia sana na kutekeleza ushauri wa mashabiki zake. Nyota anasema yeye huchukulia kila ushauri wa shabiki wake kuwa muhimu.

Kama Msanii Nyota anasema kila kitu kuhusu maisha yake kiko wazi kwa umma wala hana la siri isipokua tu "maswala ya kitandani''.

Bi Nyota anasema kila anachokiweka mtandoni kina nia ya kusaidia na kuwatia moyo wenginne, kama kioo cha jamii.