Sisi walevi hatungemsaidia Uhuru,Ruto ndiye aliyemsiaidia -Kuria (+Video)

moses Kuria
moses Kuria
Naibu wa rais ndiye aliyemsaidia rais Uhuru kushinda urais.

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amewarai wakaazi wa eneo la mlima Kenya kumpigia kura naibu wa rais William Ruto mwaka wa 2022 akisema kwamba Ruto ndiye aliyemaidia Uhuru Kenyatta kuwa rais mwaka wa 2013 na 2017 . Katika video inayosambazwa mtandaoni , Kuria anasema rais Kenyatta ‘Hangepata ushindi iwapo angewategemea walevi kama yeye kumfanyia kampeini’.

https://twitter.com/YusufJumaKenya/status/1236877498807463936

Katika video hiyo Kuria anakiri kwamba alikuwa mlevi lakini sasa ameacha pombe  na iwapo Ruto hangefanya  juhudi za  kumfanyia kampeini rais Uhuru basi hawangepata ushindi .