Siwezi kujiuzulu! Asema Kagwe

kagwe 1
kagwe 1
Waziri wa Afya  Mutahi Kagwe  amesema kwamba hatojiuzulu .

Akizungumza  katika kikao  na wanahabari huko Kisumu  siku ya jumapili  amesema kwamba ni ndoto kwa baadhi ya watu kumtaka ajiuzulu.

" Suala ambalo watu wanalitumia kunitaka nijiuzulu ni ndoto . wanaweza kuendelea kuota’ amesema

Aliendelea kusema kwamba hana mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 katika nyumba yake  .hii ni baada ya video kusambazwa mtandaoni inayodaiwa kuwa  ya mwanawe wa kiume akiwa katika karamu licha ya agizo la serikali kuzuia watu kungomana kwa hafla kama hizo.

" Kuhusu suala la video ya  mwanangu akiwa katika karamu ..sina mtoto wa kiume aliye chini ya umri wa miaka 18 katika nyumba yangu hatua inayomaanisha kwamba wote ni watu wazima .mnaweza kuwafuata na kuwauliza’ Kagwe alisema

Kuhusu suala la covid 19 nchini  Kagwe alisema vis avipya 599 vya ugonjwa huo viliripotiwa  na kufikisha jumla ya visa hivyo kuwa  6,436.

Watu 1,062 pia amepona virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona 12,961.

Hata hivyo watu 2 waliaga dunia na kufikisha jumla ya walioaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo kuwa  420