Sonko kufunguliwa mashtaka mapya ya kuwashambulia polisi Voi

Gavana wa Nairobi Mike Sonko anatarajiwa kufikishwa mahakama ya Voi ili kushtakiwa kwa makosa ya kuwashambulia maafisa wa polisi wakati alipokamatwa Disemba 6.

Sonko anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuwashambulia na kuzuia maafisa wa usalama kutekeleza wajibu wao kazini.

Kwa sasa hali ya usalama umeimarishwa huku vikosi vya polisi wakishika doria katika mahakama ya Voi.

Gavana anadaiwa 'kumpiga teke' kamanda wa polisi wa kanda ya pwani Rashid Yakubu kwenye paja lake alipokuwa akikamatwa kwenye uwanja ndege wa Ikanga.

Katika kesi hiyo, gavana atafunguliwa' shtaka la kumshambulia afisa wa polisi akiwa anatekeleza wajibu mnamo Disemba 6.''

Na shtaka la pili ni "kukataa kutiwa mbaroni na Yakubu..na kukaidi amri ya kuabiri helikopta ya polisi."

Aidha, gavana anatuhumiwa kutumia cheche za matusi kama vile," shenzi nyie, taka taka, ondoka hapa, akiwa na lengo la kuhujumu amani."

Kulingana na orodha ya mashtaka yanayomkabili yaliyoandikwa Disemba 9, Sonko anatuhumiwa kuwashambulia polisu saa 12.30 adhuhuri na kuwazuia kutekeleza wajibu wao ipassavyo kulingana na sheria za tume ya huduma za polisi 2011, ibara ya 103.

Mashahidi waliotajwa kwenye kesi hiyo ni Rashid Yakubu, Cjs James Mwanzia, Michael Muriithi, CPL Fred Sabai, CPL Stephen Mtawa, PC Ibrahim Ahmed na wengine wa serikali.