IMG_20190815_130155[1]__1565878949_72742 (3)

Sonko wa Redio Jambo azuru miji ya Kibwezi,Voi na Taveta

Sonko wa kituo cha Jambo hii leo amezuru miji iliyopo katika barabara kuu ya Nairobi kwenda Mombasa na kuwatuza mashabiki na hela kibao. Sonko huyu alianza ziara mjini Kibwezi na baadaye kuzamia Voi na kufunga ziara nzima mjini Taveta

Kituo cha Jambo kwa sasa kimemaliza mwezi mmoja katika mitaa kote nchini kikihusika katika zoezi la kuwatunuku wasikilizaji kwa ushabiki mkubwa. Kituo hiki kinawatuza mashabiki sugu wanaofahamu The Phrase That Pays Redio Jambo Ongea Usikike. Sonko wa kituo hiki alianzia juhudi hizi za mchwa viungani mwa jiji la Nairobi na baadaye akatoka jiji kuu na kuzamia miji midogo nchini.

Soma hapa:

Patanisho: Alitoka na ugali nilipoenda kumtembelea

Juma lijalo sonko huyu atazamia mji mkuu Nairobi kuwazawadi mashabiki. Sonko wa masonko atatembea viunga vya Nairobi kwa mara nyingine kwa udi na uvumba kumsaka atakayeng’amua The Phrase that Pays ambayo ni Redio Jambo Ongea Usikike.

Pata uhondo hapa:

Otile hakuninunulia gari! Jovial amwambia Massawe Jappani

 

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments