Spidi ya kifo! (+ Video )Tulimuambia asiondoke, Mashahidi wasema kumhusu jamaa aliyefariki katika ajali mbaya ya Lang’ata Road.

Ufichuzi umetolewa kuhusu  ajali mbaya ya barabarani iliyotokea mwishoni mwa wiki katika barabara ya Lang’ata iliysababisha kifo cha mwanamme mmoja .  Mashahidi  wanasema  walimshauri asiondoke  kutoka hoteli ya Weston  akiwa mlevi na atulie kidogo au atafute mtu wa kumpeleka nyumbani lakini  juhudi zao ziliambulia patupu .

https://twitter.com/YusufJumaKenya/status/1229349238301233152

Alifahamu kwamba alikuwa mlevi chakari lakini hakutaka usaidizi wa yeyote  na akaliendesha  gari la  Mercedes-Benz kwa kasi. Hatima yake  baadaye ilifahamika baada ya  gari hilo kushika  moto baada ya kugonga ua  la uwanja mdogo wa ndege wa  Wilson . Naibu OCPD wa Lang’ata John Samburumo  amesema dereva huyo alikuwa akiliendesha gari hilo kwa kasi sana .

Amesema alikuwa akitoka  hoteli ya Weston mwendo wa saa moja na dakika 20 asubuhi  na alionekana kuwa mlevi. Gari  jingine lililokuwa limeegeshwa  ndani ya uwanja wa ndege  wa Wilson pia liligongwa . Gari hilo baadaye lilishika  kasi  upande wa mbele .Mwili wake  ulipelekwa katika  hifadhi ya maiti ya City .