Spika Muturi Akasirishwa Na Wabunge Kusafiri Uholanzi Kufunzwa Upishi

Spika wa bunge Justin Muturi. | picha: the-star.co.ke | 

Spika wa bunge Justin Muturi hajafurahishwa na safari ya wabunge kadhaa kwenda nchi za Uholanzi, Ethiopia na India ambapo walifunzwa upishi.

Akihutubia bunge, Muturi alichekesha wabunge aliposema kuwa safari hizo zitafaidi sana wapishi na wafanyikazi wa mkahawa wa bunge kuliko wabunge wenyewe.

Muturi alisema kuwa wapishi na wafanyikazi hao watajifunza mengi zaidi kutoka safiri hizo kuliko wabunge wenyewe.

Muturi aliongezea kuwa ingekuwa afadhali zaidi kama wabunge wangeenda shule ya Utalii wajifunze mambo waliyokuwa wanataka kujua.

Spika alisema hayo baada ya naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya upishi na afya Benjamin Lagat, kuambia bunge kuwa kuna wabunge ambao walisafiri nje ya nchi kufunzwa kupika.

Katika taarifa iliyochapishwa na  Muturi alisema kuwa Tume ya Huduma za Wabunge itakutana siku ya Ijumaa kuangazia masuala yaliyotolewa na wabunge kuhusu ubora wa chakula kinachopikwa katika mkahawa wa bunge na hali duni ya usafi katika vyoo vya bunge.

Kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale, ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume Ya Huduma za Bunge, alilalamikia sana kuhusu chakula bungeni kuwa mbovu, vyoo kuwa chafu, na chai na vitafunio kukosa ladha.

"Lazima tuone mabadiliko katika huduma tunazopata bungeni la sivyo kamati hiyo tutaivunja tutakaporejea kutoka mapumzikoni," alisema Duale.

Soma taarifa kamili hapa