STORY ZA GHOST: Sponsor Alia Kwikwi Baada Ya Kunyang'anywa Kipusa

Ni katika kipindi tu cha Gidi na Ghost Asubuhi ambapo vioja na vituko vya kila aina hushuhudiwa. Kuanzia kauli ya waskilizaji kutoka pembe zote za Kenya, wageni na hata pia watangazaji ambao wamebarikiwa na ucheshi si haba.

Sio kila mara tunaskia kuhusu wanaume wazee almaarufu 'sponsor' ambao wana tabia za kutembea au kuchumbiana na wanadada wadogo ki umri haswa wa chuo kikuu, lakini yote unayapata katika mchuzi mtamu wa redio Jambo huku ukichanganya na kachumbari iitwayo, Patanisho.

Basi katika stori za bwana Ghost Mulee, tukio moja lililomhusisha sponsor na mpenziwe lilitokea mjini na kuwaacha wengi vinywa wazi.

Akielezea tukio hilo, Ghost alisema kuwa mwanaume mmoja alikuwa na mpenzi mmoja jijini Umoji ambaye alimfanyia kila kitu ikiwemo kumkodishia nyumba.

Huku akidhani yeye ndiye mpenzi tu wa yule kipusa, alimtembelea siku mmoja bila kumuarifu na alichokutana nacho kilimwacha akibubujikwa na machozi.

"Sasa si jamaa anajua kule ni kwake akaenda siku mmoja akipiga mbinja akija anabisha nyumba kuingia akampata mwanadada yule ametulia na jamaa mwingine kitandani akivuta sigara... hakuamini macho yake na hakuwa na la ziada ila kulia." Alisimulia bwana Ghost.

Pata uhondo kamili na tuwache tabia za sponsor jameni.

&feature=youtu.be