Tabitha Karanja wa Keroche atiwa mbaroni

TABITHA
TABITHA
Aifisa mkuu mtendaji wa Keroche Tabitha Karanja ametiwa mbaroni na makachero wa DCI katika afisi za kampuni yake eneo la Naivasha.

Maafisa wa KRA na wachunguzi wa DCI walikuwa wamepiga kambi katika majengo ya kampuni hiyo kuanzia Alhamisi asubuhi kufuatia kutolewa kwa agizo la kukamatwa kwake na mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji.

Tabitha alikamatwa pamoja na mumewe Joseph Karanja kwa madai ya ukwepaji wa ushuru wa takriban shilingi bilioni 14.

Katika taarifa siku ya Jumatano, Karanja alisema kampuni yake haijashiriki ukwepaji wowote wa ushuru na kuongeza kwamba haikua haki kwa kampuni ya Keroche “kuhujumiwa na kudhalilishwa”

Walisafirishwa kutoka Naivasha hadi makao makuu ya DCI mjini Nairobi kwa mahojiano zaidi.

Kampuni hiyo inadaiwa kukosa kulipa ushuru wa mhuri wa thamani ya bidhaa (VAT) kwa kima cha shilingi bilioni 12.34 , (milioni 329.4),kwa kinywaji cha Crescent Vodka (milioni 135.4 ) miongoni mwa bidhaa zingine.