Tafadhali Maribe tumechoka sisi!,Utapasuka msamba usipochunga

NA NICKSON TOSI

Mtangazaji wa kitambo wa runinga moja ya humu nchini Jacque Maribe amerejea tena mara hii na Denis Itumbi  baada ya kumtumia ujumbe wa kutatanisha akili za wengi siku yake ya kuzaliwa.

Jacque aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake  Instagram ambao uliwaacha wengi wakijiuliza maswali siku chache tu baada ya mpenziwe Jowie Irungu kutoka gerezani baada ya kuzuiliwa kwa takriban mwaka mmoja kutokana na madai ya kuhusishwa na kifo cha mfanyabiashara Monica Kimani.

Wengi walielekea katika mtandao huo wa Instagram na kumtaka Maribe awe wazi na kuchagua mtu mmoja baina ya Itumbi ,Erick Omondi na Jowie Irungu.

Huu ndio ujumbe aliouwandika Maribe kwa  Itumbi.

“Hakuna fasihi leo,hakuna kumbukizi za mwaka mpya,hakuna malengo ya mbeleni,lakini ni kukushukuru tu ujumbe wa urafiki ambao unasimamia ukweli na maana,kila la heri unapoadhimisha siku ya kuzaliwa muhibu''.aliandika Jacque.

Mwaka jana disemba Maribe alipokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ,Itumbi aliandika ujumbe ulioibua hisia kali miongoni mwa watu alipomtaja Maribe kama mama anayejua  kudekeza mwanamume kwa penzi ,na kusifia urembo wake alioumbwa nao Maribe.

Itumbi alitaja uhusiano wao kama kitu ambacho hakiwahi katizwa na mtu yeyote yule akisema ni urafiki uliohidhinishswa na Mola .

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya Maribe kumuarifu shabiki mmoja katika mitandao ya kijamii kuwa Yesu ndiye Bwana wake baada ya shabiki huyo kutaka ufafanuzi kutoka kwake kuhusiana na wanaume watatu ambao wote walikuwa na uhusiano  wa kimapenzi na Maribe.

“ Nasikia bwana amerudi eric nae amerudia bibi😂” aliandika shabiki.

Yesu ndiye bwana wangu ,alijibu Maribe