Tahadhari kwa wakaazi wa Lamu! KWS yasema huenda Mamba na Kiboko wakavamia makaazi yao kutokana na mvua kubwa

Shirika la wanyama pori nchini KWS sasa limewataka wakaazi wa kaunti ya Lamu kuanza kutafuta makao mbadala kutokana na mvua kubwa inayonyesha eneo hilo na kuchangia wanyama hatari wa majini kama vile Mamba,Kiboko na hata Nyoka wakiwa kwa makaazi ya wananchi kwani mafuriko yanayoshuhudiwa kaunti hiyo yatachangia wanyama hao kutoka majini.

Katika kaunti hiyo ya lamu ,vijiji kutoka lamu Magharibi katika kitongoji cha Witu vimeathirika na mafuriko makubwa huku wakaazi wa mitaa hiyo wakisema wameanza kushuhudia Kiboko wakitembea eneo hilo.

Mkuu wa KWS kaunti hiyo Mathias Mwavita amesema ripoti imewasiilisha kwa afisi yake kuhusiana na Kiboko hao na wameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanakabiliana nao kabla ya kudhuru maisha ya binadamu.

Wanyama hao hatari sasa wanasemekana kuwa wanatoka katika mto Tana kutokana na mto huo kufurika na kuvunja kingo zake.

Mwavita amewaonya watoto na wakaazi wa eneo hilo dhidi ya kuogelea katika mito iliyoko karibu akisema huenda wakashambuliwa na wanyama hao..

"Floods have caused a lot suffering and unfortunately, that includes wild animals that are also finding themselves in human habitats. We need to be vigilant to stay safe.""Keep away from all water bodies as they are possibly hiding there. We have, however, deployed officers to help the affected villages,” Mwavita amesema.

Wanawake pia wameonywa dhidi ya kuosha nguo zao karibu na mito ama mabwawa.

Amewahimiza wakaazi wa Lamu dhidi ya kujenga nyumba karibu na mito kwa kile amesema ni rahisi kuingiliwa na wanyama hatari wa majini.

“Many of these problems are created by us. People have encroached into wildlife reserves and set up homes without thinking about where these animals will go. Even as we help you, stop inviting trouble and obey the law,” Mwavita alionya.