imgonline-com-ua-CompressToSize-CFYzmqc26YUBm8PX

Taharuki kijijini baada ya mvua kufukua mifupa ya binadamu wasiyemtambua

Athari za mvua kubwa yasababisha mmonyoko wa udongo na kufukua mifupa ya binadamu  na kuwatia wakaazi woga.

Mvua kubwa inayonyesha katika maeneo mengi nchini Kenya inatarajiwa kuongezeka katika kipindi cha miezi miwili huku mmomonyoko wa udongo na mafuriko yakishuhudiwa.

Wanakijiji wa lokesheni ya Kimalel Baringo kusini walistaajabu baada ya kupata mifupa ya binadamu anayeaminika kuzikwa miaka mingi iliyopita.

Maeneo Mengi Kushuhudia Mafuriko, Huku Idara Ikionya Mvua Kuendelea

Wakaazi wanasema kwamba mifupa hiyo ya binadamu inakisiwa kusombwa na maji ya mafuriko kwa kuwa wenyeji hawana uhakika iwapo palikuwa na jamii iliyozika maneeo hayo.

Wanasema kwamba wameshindwa kutambua familia ambayo walihusika katika kuzika jamaa yao katika eneo hilo.

Baadhi ya wanakijiji wanasema kwamba tukio hilo ni la ajabu sana na linafaa kufanyiwa tambiko ili lisije likadhuru watu wa eneo hilo.

“Mifupa hiyo ya binadamu ilipatikana katika mtaro wenye kimo cha futi saba kwenda chini, hata hivyo haijulikani miaka mabyo mwili huo ulizikwa” wakaazi walisema.

Mzee Wa Miaka 94, Wake 19 Na Watoto 100 Aoa Tena, Kunani ?

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments