Takriban watumishi wa umma elfu 60 kustaafu - 2020

Waziri wa Utumishio kwa umma Margaret Kobia
Waziri wa Utumishio kwa umma Margaret Kobia
Tume ya utumishi kwa umma inakabiliwa na changamoto za kupata fedha ili kuajiri wafanyikazi 33,792.

Idara hiyo inasema inahitaji kwa dharura shilingi bilioni 15.6 kuajiri wafanyikazi wapya, 26,792 katika daraja la chini kwa kima cha shilingi bilioni 12.1 na maafisa 7,000 wa magereza kwa shilingi bilioni 3.5.

Tayari kuna kunafasi wazi 17,214 katika utumishi wa umma na 4,080 katika idara ya magereza.

Takriban maafisa 22,981wanatarajiwa kupandishwa ngazi zoezi ambalo litagharimu shilingi bilioni 3.7. Jumla ya maafisa 11,761 wa magereza pia wanasubiri kupandishwa vyeo na kugharimu shilingi bilioni 1.2.

Katibu wa utawala katika wizara ya utumishi kwa umma Mary Kimonye aliambia kundi la wabunge kwamba nafasi hizi zimetokana na kuzeeka kwa baadhi ya wafanyikazi.

Alitowa wito kwa kamati ya bunge ya Utawala na Usalama wa kitaifa chini uwenyekiti wa mbunge wa Kiambaa Paul Koinange kutenga pesa kwa jukumu hilo.

Kamati za bunge zinatarajiwa kuwasilisha bajeti zao kwa kamati kuu ya bajeti hapo kesho.

Kamati ya bajeti ikiongozwa na Kimani Ichungwa kisha itawasiliha bungeni makadirio ya matumizi ya pesa za serikali bungeni Juni 4.

Takwimu katika hazina ya kitaifa zaonyesha kwamba wafanyikazi wa umma 59,400 kati ya 500,000 watastaafu ifikiapo Juni 2020. Wengi wa watakao staafu ni wa daraja za juu, mameneja na maafisa wa kiufundi.

Huenda serikali ikalazimika kusalia na baadhi ya maafisa kutoka na ujunzi wao kazini.

NA MOSES ALIWA